Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie
Brandts amesema bado anahitaji mshambuliaji mwenye uwezo wa juu ili kusaidia
katika kikosi chake.
Brandts ambaye ameelezwa
kutofurahishwa na kiwango cha Mnigeria Brendan Ogbu, amesema lazima Yanga
usajili mshambuliaji na mchakato unaendelea.
“Kweli bado tunatafuta
mshambuliaji, muda unaturuhusu lakini tunajitahidi kufanya haraka kwa kuwa
lazima tumpate mshambuliaji wa kimataifa na mwenye uwezo ambao unaonekana ni
tofauti au wa ziada.
“Si vizuri kupata mshambuliaji
ambaye tunaona uwezo wake hauna tofauti na wachezaji wa hapa nyumbani,”
alisema.
Mholanzi huyo alisema Yanga
inalazimika kuimarisha ulinzi na kuongeza
nguvu ya ushambuliaji kwa kuwa itashiriki katika michuano ya kimataifa.
Aidha, Brandts amesisitiza
wachezaji wa Yanga wanapaswa kujua kuwa msimu ujao utakuwa mgumu kwao kwa kuwa
ni mabingwa.
“Unapokuwa juu kila mmoja
anapania kukushuka, hivyo kila mechi ya Yanga itakuwa ngumu na yenye ushindani
maradufu.
“Wachezaji wangu
nimezungumza nao lakini bado nawasisitiza lazima wajitume zaidi na wapambane
maana msimu ujao ni mgumu sana kwetu,” alisema Brandts.
0 COMMENTS:
Post a Comment