July 29, 2013


Uamuzi wa mshambuliaji nyota wa PSG, Zlatan Ibrahimovic kuvua bukta na jezi na kubaki na nguo za ndani wakati wa mechi yao ya kirafiki dhidi ya Real Madrid kumezua gumzo.

Mswidi huyo alifanya hivyo mara tu baada ya mechi kwisha baada ya kuamua kubadilishana jezi na mchezaji wa Madrid na kugawa bukta yake kwa mashabiki.

Mitandao imekuwa ikijadili kwamba uvaaji wa wachezaji umekuwa hauna tofauti na ule wa bikini wanaovaa kinadada hasa wanapokuwa wanaogelea.


Baadhi ya mitandao ya Hispania na Sweden ndiyo imeongoza zaidi kwa kulichambua suala hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic