July 29, 2013


Klabu ya Napoli imeamua kuandaa pati binge la pati kwa ajili ya mshambuliaji wake mpya Gonzalo Higuaín.

 Higuain amejiunga na Napoli akitokea Madrid na mashabiki wengi wa timu hiyo ya Italia wameonyesha kufurahishwa na uhamisho wa Muaegentina huyo.

Taarifa kutoka katika klabu hiyo zimeeleza kuwa Higuain atapokelewa na Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis leo usiku kwenye Uwanja wa San Paolo.

Tayari matangazo yamesambazwa katika mji wa Napoli kuelezea ujio wa Higuain ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina.

Pamoja na Higuain, Napoli pia imewasajili wachezaji José Callejón na Raúl Albiol ambao msimu huu watapambana kutwaa taji la Serie A badala ya La Liga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic