July 29, 2013


Kocha Mkuu wa The Cranes, Milutin Sredojevic ‘Micho’ amesema mara tu baada ya ushindi wa bao 1-0 jijini Dar, alijua lazima wataitoa Taifa Stars.

The Cranes imeing’oa Taifa Stars kwa kuichapa jumla ya mabao 4-1 katika mechi mbili za kuwania kucheza fainali za Chan nchini Afrika Kusini.

Micho amesema Stars ni timu nzuri lakini ina nguvu upande mmoja tu pia ni lahisi kuizuia kama kutakuwa na mpango madhubiti kumkamata Ngassa.

“Tulifanya kazi ya ziada mimi na Timbe, lengo lilikuwa ni kuangalia njia za Ngassa, ndiyo maana utaona hakuwa tatizo katika mechi zote mbili.

“Siwezi kusema kila kitu, lakini tulimzuia kwa aina ambayo ilikuwa ni vigumu sana kujua, siwezi kusema kila kitu.

“Ila ushauri wangu kwa Stars ni lazima wajenge kuwa na njia za ziada za ushambuliaji. Ukiangalia katika mechi ya kwanza Dar es Salaam, tungeweza kushinda hata zaidi ya bao 1-0,” alisema Micho.

Mara ya mwisho Stars kwenda Chan ilikuwa mwaka 2009 katika michuano iliyofanyika nchini Ivory Coast lakini ikaishia katika hatua ya robo fainali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Zambia mjini Bouake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic