July 24, 2013



Bayern Munich imeonyesha kweli wao ni wababe wa Barcelona baada ya kuwachapa kwa mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Allianz Arena jijini Munich, leo.

Kocha mpya, Pep Guardiola ameiongoza Bayern kuibuka na ushindi huo dhidi ya timu yake ya zamani huku mshambuliaji nyota duniani, Lionel Messi akishindwa ‘kucheka’ na yavu.

Philipp Lahm ndiye alifunga bao la kwanza katika dakika ya 14 kabla ya bao la pili la Mario Mandzukic katika dakika ya 87.
Bayern ndiyo iliyoing’oa kwa aibu Barca katika michuano ya Ligi ya Mabinwa Ulaya tena kwa aibu baada ya kuichapa kwa jumla ya mabao 7-0.

Barca iliyokuwa chini ya kocha msaidizi, Jordi Roura ilionyesha uwezo lakini Wajerumani hao ambao ndiyo mabingwa wa dunia walikuwa imara zaidi.

VIKOSI:
Bayern Munich: Neuer (Starke 46), Rafinha, Dante (Van Buyten 59), Boateng, Alaba, Thiago, Lahm (Gustavo 59), Kroos, Ribery, Robben (Shaqiri 46), Muller (Mandzukic 46).
Mabao: Lahm 14, Mandzukic 87.
Barcelona: Pinto (Oier 46), Montoya (Kiko 46), Bartra (Gomez 46), Mascherano (Planas 46), Adriano (Patric 46), Song (Espinosa 46), Sergi Roberto (Ilie 46), Dos Santos (Quintilla 46), Tello (Joan Roman 46), Messi (Dongou 46), Alexis (Dani Nieto 46).





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic