Sunderland imeitoa shoo Tottenham katika michuano ya Barclays Asia inayofanyika nchini Hong Kong kwa kuichapa kwa mabao 3-1.
Pamoja na kipigo hicho,Tottenham ilipata pigo baada ya beki wake Jan Vertonghen kuumia na kulazimika kukimbizwa hospitali.
Mechi hiyo ililazimika kupunguzwa muda katika kipindi cha pili hadi dakika 40 kutokana na hali mbaya ya hewa.
Timu hizo chini ya makocha Andre Villas-Boas na Paolo Di Canio zilionyesha soka la ushindani mkubwa na mabao ya Sunderland yakafungwa na Cabral 34, Brown 64, Karlsson 80, wakati Sigurdsson ndiye aliwafuta machozi Spurs katika dakika ya 28.
TOTTENHAM: Gomes (Friedel 41); Walker, Dawson, Caulker (Vertonghen 41, Fryers 49), Rose; Lennon (Defoe 41), Parker, Huddlestone (Carroll 70), Sigurdsson; Adebayor, Dempsey (Townsend 70). Subs: Lloris, Naughton, Assou-Ekotto, Fryers.
Mfungaji: Sigurdsson 28
SUNDERLAND: Mannone; Gardner, O’Shea, Brown (Roberge 77), Colback; Johnson (Karlsson 62), Cabral, Giaccherini Larsson (Ba 62); Altidore (Wickham 73), Sessegnon. Subs: Pickford, Westwood, Vaughan, Mandron, McClean, Cuellar.
Wafungaji: Cabral 34, Brown 64, Karlsson 80
Refa: Liu Kwok Man
0 COMMENTS:
Post a Comment