July 24, 2013


Baada ya kupoteza mechi mbili za kirafiki nchini Afrika Kusini, Kocha Manuel Pellegrini amerejea kutoka katika msiba wa mama yake mzazi na kukisaidia kikosi chake kushinda kwa bao 1-0 mechi ya kirafiki dhidi ya South China.

Pellegrini alilazimika kurejea kwao Chile kwa ajili ya msiba wa Silvia, kabla ya kuungana na City na kuingoza kushinda.


Kocha huyo aliamua kusafiri kwa saa 24 kuiwahi mechi hiyo baada ya kutoka msibani, hali iliyoonyesha alipania kurekebisha mambo kadhaa baada ya vipigo vya nchini Afrika Kusini.

Bao pekee katika mchezo huo uliokuwa wa kukata na shika lilifungwa na Dzeko ambaye alitolewa katika dakika ya 75 na nafasi yake kuchukuliwa na Richards.

South China: Barry, Chak, Ticao, Cheng (Martins, 45), Naves, Lee Wai Lim (Lee Hong Lim, 52), Sealy, Tse, Joel, Kwok, Zhang
Man City: Hart, Zabaleta (Sinclair, 75), Kompany, Lescott, Clichy (Kolarov, 45), Milner, Nasri, Barry (Rodwell, 55), Fernandinho (Javi Garcia, 65), Toure (Negredo, 55), Dzeko (Richards, 75)
Bao: Dzeko

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic