Watu 95,000 wamemshuhudia mshambuliaji wa Liverpool, Luiz Suarez akiichezea timu yake hiyo kwa mara nyingine tena katika mechi ya kirafiki.
Mashabiki hao kwenye Uwanja wa MCG jijini Melbourne, Austtalia walimshuhudia Suarez akiisadia Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Melbourne lakini nahodha Steven Gerrard na Aspas ndiyo wakafanya kazi ya kufunga mabao.
Suarez ambaye hakuichezea Liverpool tokea alipomng’ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic mwishoni mwa msimu uliopita alikuwa msumbufu kwa mabeki wa Melbourne.
Hata baada ya kumg’ata Ivanovic na kufungiwa, Suarez alishindwa kutulia na Liverpool baada ya kuwa gumzo la usajili.
Arsenal na Real Madrid zilionyesha nia ya kutaka kumsajili lakini mwisho zinaonekana kushindwa.
VIKOSI:
Melbourne: Coe; Ansell, Broxham, Nabbout, Celeski; James Jeggo, Pain, Makarounas, Leijer; Galloway, Geria.
Liverpool: Jones (Mignolet 72), Johnson (Kelly 72), Skrtel (Coates 72), Wisdom (Agger 72), Enrique (Flanagan 72), Gerrard (Lucas 64), Allen (Spearing 72), Henderson (Luis Alberto 72), Ibe (Downing 72), Sterling (Aspas 72), Borini (Aspas 72).
Mabao: Gerrard 32, Aspas 90+2
Waliobadilishwa: Mignolet, Kelly, Coates, Agger, Flanagan, Spearing, Lucas, Downing, Alberto, Aspas, Suarez, Robinson, Assaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment