July 23, 2013



  Pamoja na kuonyesha ni mwenye imani kali ya dini ya Kiislam lakini picha zinazomuonyesha mshambuliaji Papis Cicce wa Newcastle akiwa Casino zimezua zogo kubwa.

Cisse raia wa Senegal amekuwa akiupa wakati mgumu uongozi wa Newcastle hasa katika suala la kuvaa jezi ya wadhamini wao Wonga ambao kazi yao ni ukopeshaji na wanajiendeleza kwa kupata riba na dini tukufu ya Kiislam inatakaza.


Lakini picha hiyo inamuonyesha Cisse akiwa amejifunika karibu kabisa na meza ya kucheza kamari akiendelea kucheza.

Hata hivyo inaonekana ubora wa picha yenyewe unaweza kumfanya Cisse aikane picha yenyewe kwamba si yeye.

Imeelezwa wakati akiwa casino, Cisse alikuwa akicheza kamari ya fedha kiasi cha chini kuanzia pauni 10 hadi 30, na inaonekana alifanya hivyo wengi wasijue kama ni yeye.

Bado suala hilo linaonyesha linataka uthibitisho kwa kuwa picha hiyo haina ubora zaidi.
Hivi karibu, Newcastle ililazimika kumpa nafasi afanye mazoezi peke yake baada ya kugoma kuvaa jezi zenye nembo ya Wonga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic