Uongozi
wa klabu ya Yanga leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu ya urushwaji
wa michezo yake ya Ligi Kuu katika kituo cha luninga cha Azam ambacho kimeingia
makubaliano na kamati ya Ligi Kuu kuonyeshwa michezo yote ya ligi kwa
kipindi cha miaka miatatu (3).
Akiongea
na waandishi wa habari mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji amesema uamuzi
wa kamati ya ligi kuingia mkataba na kituo cha Azam Tv bila ya kuwashirikisha
wahusika wenyewe ambao ni vilabu vishiriki haukuwa sawa.
Sisi kama
klabu ya Yanga tulikaa kikao cha kamati ya utendaji na kuona taratibu za kupewa
haki ya matangazo kwa kampuni ya Azam haikua sawa, sisi viongozi wa kalbu ya
Yanga hatukushirikishwa katika mchakato huo hivyo tukaona ni vema tuje kwa
vyombo vya habari tuulezee umma juu ya maazimio ya kamati ya utendaji.
Ifuatayo
ni taarifa kamili kwa vyombo vya habari:
YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.
Hivi
karibuni, Tanzania Football Federation (TFF) iliunda Tanzania Premier
League chini ya Bodi yampitoBodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi
itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake kuingia
katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo
ina mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football Club). Makubaliano
ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam Television, Kamati ya Utendaji ya
YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika misingi ifuatayo:
1. BODI YA TPL
1.1 Bodi iliyoko sasa hivi ni ya mpito ambayo
ilitakiwa kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi
wa tarehe ……….. mwaka huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka
mingi wakati inakaribia kuondoka katika ofisi.
1.2 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa
kidemokrasia.
1.3 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe
hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.
2. UTARATIBU WA DUNIA NZIMA
2.1 Haijawahi kutokea katika ligi ya mpira wa
miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana katika ligi kuachia haki
zake za urushwaji wa michezo zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya
upinzani.
2.2 Mfumo (undertaking) ambao TPL inataka
kuanzisha kwa njia ya kulazimisha mkataba kwa YANGA iachie urushwaji wa
michezo yake ya soka yarushwe na Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa
ushindani katika soka ya Tanzania.
2.3 Makubalianokati ya TPL na Azam Television
kuhusu utaratibu wa malipo yanasemakwamba Klabu ya YANGA na Klabu zingine
zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania watapata mgao sawa wa mapato
ya urushwaji wa michezo hii, ambayo YANGA inapinga kwa sababu kama
inavyofanyika duniani kote kwenye ligi zilizofanikiwa (angalau) kutofautisha
mgawanyo wa mapato kati ya timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa ligi.
2.4 Kamati ya Utendaji ya YANGA siyo tu
haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato ambao hautofautishi kati ya timu ya
kwanza katika ligi na timu ya mwisho katika ligi, lakini pia ukosefu wa viwango
(premiums) vitakavyolipwa:
2.4.1 Vilabu vya mpira vyenye ufuasi wa washabiki
wengi;
2.4.2 Vilabu vya mpira vinavyoendeshwa na
Wanachama;
2.4.3 Vilabu vya mpira visivyopata ruzuku kutoka
Serikalini n.k.
3. MIGOGORO YA MASLAHI
3.1 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL ni
Mkurugenzi mwandamizi wa Makampuni ya Azam na kwa hivyo mazungumzo ya
siri kati ya Bodi ya TPL na Azam ni ya kutiliwa mashaka.
3.2 Makampuni ya Azam yana yanashindana
kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya utengenezaji wa vinywaji baridi na
imeonyesha huko awali inaweka “matakwa maalum” muhimu zaidi kuliko mprira
wa miguu, kama vile Azam F.C. hawashiriki katika Kombe la Tusker na kwa
hiyo YANGA inakuwa na msimamo kwamba kwa Azam Television kupewa leseni ya
kurusha matangazo ya mpira wa miguu inatishia biashara za washiriki wa sasa na
wa baadaye wa YANGA.
3.3 Azam na YANGA wana uadui wa kimichezo.
Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA alipotaka kwenda YANGA, Azam F.C. walimkopesha
kwa nguvu kwa Klabu ya Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika kwa matangazo yenye
upendeleo kama Azam Television itarusha hewani michezo yake n.k.
4. KUTOKUWA NA UWAZI
4.1 Mkataba wa utangazaji wa miaka mingi
unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao badohaujarushwa Television ya Azam
haukushindanishwa na vyombo vingi vya habari, na vyombo ambayo wako
tayari kwenye soka havikujulishwa kuhusu fursa hii au walizuiliwa kufikisha
mapendekezo yao ya maombi ya haki za kurusha matangazo katika Ligi Kuu
(Tanzania Premier League).
4.2 Ukosefu wa uwazi wa TPL unanonyesha kuwa MoU
iliyokusudiwa kuwekewa saini na TPL haikufikishwa YANGA kwa ajili ya mapitio ya
kisheria, licha ya YANGA kufanya ombi hilo kwaTPL.
5. MAZINGATIO YA KIBIASHARA
5.1 Mamlaka ya kuamua mzozo wowote wa mkataba wa
leseni ya utangazaji wa Ligi Kuu (Tanzania Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama
ya kisheria na siyo FIFA. TPL inasingizia kwamba leseni ya matangazo
ambayo inakusudia kufanya kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa
kuukubali "lock, stock and barrel."
5.2 TPL inaelezea kimakosa makubaliano ya leseni
ya urushaji wa mchezo ya mpira inayotarajia kuingia na Television ya Azam
kama "makubaliano ya udhamini" (“sponsorship agreement”) ambayo siyo
sahihi, kwa sababu urushaji wa michezo ya mpira wa miguu ni biashara
inayotokana na maslahi ya uhusiano na hivyo
wahusika
wote ni lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.
Kwa
mfano, moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni mapato ya kiingilio ya
mlangoni yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo urushwaji wa michezo
hii itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya YANGA Dar es Salaam
huingiza makusanyo ya mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila mchezo na hata
kushuka kidogo kwa 25% katika mahudhurio ya mechi za YANGA zinafikia mara mbili
ya mapendekezo ya mapato takribani Sh milioni 8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA
kutoka mradi wa kibiashara kati ya TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya,
kwamba hata siku za nyuma kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira
unapochezwa, wadau wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji)
walikuwa wanaafikiana kwanza kwa pamoja kuhusu mapato na mgawanyo wake.
Kamati ya
Utendaji ya YANGA ina maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara yanayoihusu
ni lazima iyalinde maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo makubaliano ya TPL /
Azam Television hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA haitaki
mchezo wake urushwe hewani na Azam Television.
Msisitizo
wa TPL kuwa lazima Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA
linasikitisha. Kamati ya Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu vingine vya
mpira wa miguu zikiruhusu michezo yao kurushwa na Azam Television ila
haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mchezo wake wa Vodacom Premier
League katika Azam Television.
………………………………………..
(YUSUF
MANJI)
MWENYEKITI
YOUNG
AFRICANS SPORTS CLUB
31 JULAI,
2013
0 COMMENTS:
Post a Comment