Kwa mara ya kwanza, Lionel Messi na Neymar wamekichezea timu moja ndani ya kikosi cha Barcelona na timu hiyo imetoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Lechia Gdansk.
Mechi hiyo ni ya kwanza kwa Neymar ambaye mejiunga na timu hiyo akitiokea Santos ya kwao Brazil.
Hata hivyo wawili hao hawakucheza pamoja baada ya Messi kutoka na Neymar aliingia naye lakini akichukua nafasi ya Alexis.
Katika mechi hiyo ya kwanya Neymar hakufunga bao lakini Messi ndiye aliikomboa Barca kwa kufunga bao la kusawazisha.
Wawili hao kuwa katika kikosi kimoja limekuwa gumzo kubwa katika mchezo wa soka duniani huku baadhi ya wadau wakiamini hawawezi kufanya vizuri wakiwa pamoja.









0 COMMENTS:
Post a Comment