Hatimaye mshambuliaji
nyota, Neymar ametua leo jijini Barcelona na kujiunga na timu yake mpya.
Neymar raia
wa Brazil atajiunga na wenzake na kuanza mazoezi kesho Jumatatu ikiwa ni mara
ya kwanza tokea ajiunge na timu hiyo.
Kupitia mtandao
wa kijamii wa Instagram, Neymar aliweka picha yake mara tu baada ya kutua
jijini Barcelona na kuandika "Bom dia / Buenos días".
Hayo ni
maneno ya Kireno na Kihispania, yakimaanidha “Habari za asubuhi”, kuonyesha
amewasili Barcelona asubuhi na mapema.
Kutua kwa
mshambuliaji huyo, ni faraja nyingine kwa Barcelona ambayo imetoko ziarani
nchini Norway na kutoa kipigo cha mabao 7-0.
Neymar
amekuwa gumzo baada ya kuisaidia Brazil kutwaa Kombe la Mabara huku akiibuka
mfungaji na mchezaji bora ikiwa ni siku chache baada ya kujiunga na Mabingwa hao wa Hispania.
Gumzo
linaongezeka kama kweli ataweza kucheza vizuri kwa kushirikiana na nyota
mwingine Lionel Messi raia wa Argentina.
0 COMMENTS:
Post a Comment