Yametimia, hatimaye Gerardo 'Tata' Martino amekabidhiwa timu kama kocha mpya wa Barcelona.
Barcelona iko nchini humo kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki ikiwa ni moja ya sehemu ya ziara yake katika nchi mbalimbali za Ulaya.
VILANOVA NA BENCHI LAKE LA UFUNDI |
Tata ambaye alitangazwa kuwa kocha mpya wa Barcelona, takriban kilomita 2,573 kutoka Oslo, Norway jana alitua jijini humo na kukabidhiwa mikoba iliyokuwa inashikiliwa na Tito Vilanova aliyekuwa mgonjwa.
Tata raia wa Argentina aliungana na memba wengine wa benchi la ufundi akiwemo kocha msaidizi Jordi Roura na Francesc Ferrer 'Rubi'.
HA
Hii maana yake Barcelona imeanza kazi na kocha mpya ingawa wadau wamekuwa na hofu huenda ikaanza kila kitu upya.
Tata amewahi kufanya vizuri akiwa na Newell Old Boys na timu ya taifa ya Paraguay, sasa anachukua nafasi ya Vilanova ambaye hali ya afya yake imekuwa ikizidi kudhoofika.
0 COMMENTS:
Post a Comment