Picha ya Lionel Messi akiwa na bonge la mama, imezua gumzo kubwa baada ya kuchapishwa na gazeti moja maarufu la udaku nchini Argentina.
Gazeti la Pronto limeitumia picha ya Messi akiwa katika klabu ya usiku ya 'Night of chaos’ ya jijini Las Vegas nchini Marekani.'
Ingawa Messi hajazungumza lolote kuhusiana na picha hiyo, lakini inamuonyesha akiwa ni mtu mwenye hofu baada ya kukumbatiwa.
Mwanamke mwenye umbo kubwa aliyemkumbatia alikuwa amesimama, wakati nyota huyo maarufu zaidi katika soka katika kipindi hikiwa amekaa amekaa.
Huenda picha hiyo ikaleta matatizo makubwa kati ya Messi na mpenzi wake Antonella Roccuzzo ambaye sasa analea mtoto wa miezi tisa aitwaye Thiago.
Messi amekuwa akisifiwa kutokana na kutoshiriki katika masuala yoyote yanayohusisha kashfa, ikiwa ni pamoja na kuwa na mapenzi makubwa na familia yake.
Hivi karibuni, pamoja na kuchukua uamuzi wa kujifungua mtoto na Antonella aliyekuwa mpenzi wake tokea akiwa shule, lakini alijichora tatuu yenye mikono na jina la mwanaye Thiago.
0 COMMENTS:
Post a Comment