August 1, 2013


Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amepata tatuu ya uzeeni kwa kulipa pauni 80 au Sh 200,000 za Kibongo.

Mourinho ameamua kuchora tatuu hiyo yenye maneno matatu ambayo ni majina ya watu wa familia yake.

Kocha huyo Mreno mwenye vituko ameandika tatuu hiyo katika mkono wake wa kushoto ambayo ni majina matatu ya mkewe (Tami), binti yake (Tita) na mtoto wa kiume (Zuca) ambaye ni wa mwisho.


Hata hivyo kocha huyo hajatoa maelezo kuwa kwa nini amefanya hivyo lakini tatuu hiyo mpya imeonekana wakati akiwa bize na Chelsea yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic