VIONGOZI wa
matawi ya wanachama wa klabu ya Yanga SC, hatimaye wamemuunga mkono mwenyekiti
wa timu hiyo, Yusuf Manji kufuatia kauli yake ya kupinga kusaini mkataba wa
makubaliano ya mechi zao kurushwa hewani na TV ya Azam.
Baadhi ya viongozi wa matawi na wanahabari wakifuatilia kikao hicho. |
Viongozi wa matawi ya Yanga wakishangilia baada ya uamuzi huo kutolewa. |
Akizungumza
kwa niaba ya viongozi hao, Bakili Makele alisema kuwa, wanaunga mkono uamuzi wa
timu hiyo kupitia kwa Mwenyekiti wao kutokana na kujiridhisha baadhi ya dosari
zilizoainishwa kwenye kikao cha kamati kuu ya timu yao. Pia amemuomba Rais wa
Shirikisho la soka nchini (TFF), Leodgar Tenga kuingilia kati suala hili mama
matawi ya Yanga yote nchini hayako tayari kuruhusu Azam kuonyesha mechi za timu
yao.
0 COMMENTS:
Post a Comment