July 31, 2013


...AKIITUMIKIA SIMBA


Pamoja na kuingia doa kwa kulambwa kadi nyekundu katika mechi yake ya kwanza jijini Dar akiwa na Simba, Betram Mwemboki amepewa ulaji
Mwombeki, Mtanzania aliyekuwa akisaka maisha nchini Marekani amesajiliwa leo kwa miaka miwili na Msimbazi.
 
..AKISAINI MBELE YA MZEE KINESI

Mshambuliaji huyo aliyewahi kuichezea Pamba ya Mwanza alilambwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya URA ya Uganda ikiwa ni dakika chache baada ya kuifungia Simba bao.

Baada ya kutolewa kwake, Simba ilimaliza mchezo huo ikiwa imelala kwa mabao 2-1 kutoka kwa Waganda hao walioendeleza rekodi ya kutofungwa na Simba.
 
AKIWA MAZOEZINI NA SIMBA (WA KWANZA KULIA)

Lakini Mwombeki alionyesha uwezo mkubwa katika dakika hizo chake alizocheza na beki wa URA, Joseph Owino akamsifia na kuwataka Simba kutopoteza nafasi na badala yake wamuwahi mara moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic