Kiungo
nyota wa Arsenal, Mikel Arteta atakuwa nje ya kikosi hicho kwa mwezi mmoja na
nusu.
Muda
huo utaanzia kesho wakati Arsenal itakapoanza mapambano ya Ligi Kuu England kuhakikisha
inatwaa ubingwa huo ambao imekuwa ikiutafuta kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
Kocha
Mkuu we Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha nahodha wake huyo msaidizi raia ya
Hispania ni majeruhi baada ya kuumia mazoezini.
Hali
hiyo inaifanya Arsenal kuwa timu inayoandamwa na majeruhi zaidi kuliko nyingine
zote.
Tayari
zaidi ya wachezaji saba wa kikosi cha kwanza ni majeruhi na Arsenal itaanza
ligi dhidi ya Crystal Palace ambayo ndiyo imerejea tena ligi kuu hiyo kesho.
Hali
hiyo imekuwa ikiwapa hofu kubwa mashabiki wa Arsenal ambao wakati wa msimu wa
usajili hawakusajili hata mchezaji mmoja mzoefu au maarufu.
0 COMMENTS:
Post a Comment