Siku chache baada ya kurejea Yanga,
Mshambuliaji Hamis Kiiza amepata timu inayotaka aende nchini Lebanon kwa ajili
ya kucheza soka la kulipwa.
Uongozi wa Yanga umeonyesha uko tayari
kumuachia iwapo kila kitu kitakwenda vizuri na kufuata utaratibu unaotakiwa.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga,
Abdallah Bin Kleb ambaye hushughulikia masuala ya usajili ya Yanga, amesema
tayari wameishaijibu barua.
“Tayari uongozi unashughulika na suala
hilo na umeihoji timu hiyo kama kweli inamtaka Kiiza kwa ajili ya majaribio au
kumnunua. Maana kidogo barua yao hatujaielewa vizuri,” alisema.
Uongozi wa Yanga hautakuwa na kinyongo
kumuachia Kiiza kama klabu hiyo itatoa ofa nzuri lakini pia tutazungumza na
mchezaji mwenye kama atakubali, basi tutafanya hivyo.
Kiiza ameanza mazoezi ndani ya siku
chache tu akiwa amerejea nchini akitokea Uganda baada ya kutaka apewe dau la
dola 50,000. Hata hivyo uongozi wa Yanga ulimpa dau la dola 35,000.
Tayari Kiiza ameanza mazoezi na kikosi
cha Yanga chini ya Brandts, hata hivyo amekuwa akionekana hayuko fiti, jambo
linaloashiria hakuwa akifanya mazoezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment