August 29, 2013




Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema mwamuzi Martin Saanya aliyechezesha mechi yao dhidi ya Coastal Union ndiye alikuwa nyota wa mchezo huo.

Brandts raia wa Uholanzi alisema ‘aliwauma’ na alichezesha kwa kubabaika tokea mwanzo.
“Maamuzi yake mengi yalikuwa yasiyokuwa na uhakika na alionekana alikuwa anatafuta kitu fulani.


“Kama utaambiwa uchague mtu aliyeng’ara leo basi ni yeye maana mambo yake mengi yalikuwa ni ya kubabaisha tu,” alisema Brandts.
“Sipendi kuzungumzia waamuzi, lakini mwamuzi wa leo ametia for a na mwisho amefanikiwa kutoa penalti.”
Saanya alitoa penalti katika dakika ya 90 na nahodha Jerry Santo akafunga bao la kusawazisha.
Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 na kuzifanya timu zote mbili zilizoanza na ushindi katika mechi za kwanza kufikisha pointi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic