Kiungo wa Arsena, Alex
Oxlade-Chamberlain atakaa nje kwa wiki sita kutokana na kuwa majeruhi.
Chamberlain analazimika kukaa mwezi mmoja na nusu bila ya
kuitumikia Arsenal kutokana na kuumia goti.
Kutokana na hali hiyo, Chamberlain ataikosa
timu ya taifa ya England na tayari Kocha Mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger,
amethibitisha kiungo wake ni majeruhi.
Chamberlain, 20, aliumia katika mechi
ya kwanza ya Ligi Kuu England, msimu huu ambayo ilikuwa ni dhidi ya Aston Villa
na Arsenal ikalala kwa mabao 3-1.
Hatari zaidi kwa Arsenal ni kwamba
itawakosa wachezaji wengine muhimu na inakabiriwa na mechi muhimu ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya dhidi ya Fenerbahce ya Uturuki.
0 COMMENTS:
Post a Comment