
Lucy Mgina
na Martha Mboma
KIPA wa Taifa Stars, Juma Kaseja amesema
ameshindwa kusaini mkataba wa kujiunga na FC Lupopo ya DR Congo kwa kuwa
wahusika wa klabu hiyo walimkabidhi ukiwa umeandikwa kwa Lugha ya Kifaransa.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kaseja
alisema alipelekewa mkataba ambao alitakiwa kuusaini, baada ya kuuangalia akiwa
na watu wake wanaomsimamia, wakakuta umeandikwa kwa Lugha ya Kifaransa ambayo
wao hawaifahamu.
“Mkataba ulikuja kwa Kifaransa, tukawataka
wakautafsiri kwa lugha ambayo sisi tutaielewa kisha waulete tena ili uonyeshe
yale tuliyoyataka kama yamo.
“Kuna watu wananisimamia kila kitu katika hili
na ilikuwa ngumu kusaini kwa kuwa hatujui kilichoandikwa kwa sababu kuna mambo
inabidi tuyaelewe kabla sijasaini,” alisema Kaseja ambaye ni kipa wa zamani wa
Simba.







0 COMMENTS:
Post a Comment