Richard Bukos na Lucy Mgina
KOCHA wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime amesema
sababu kubwa ya kumsajili mshambuliaji Musa Hassan Mgosi (pichani) ni kuimarisha safu
yake ya ushambuliaji lakini atamtumia zaidi kama mwalimu kwa wenzake kwa kuwa
yeye ni mzoefu.
Maxime amesema kuwa ana imani Mgosi atatumia
uzoefu wake kuwa kioo kwa wenzake hasa chipukizi ili kuipa faida klabu hiyo. Nimeamua
kuwachukua wachezaji kadhaa wakongwe akiwemo Mgosi ambaye hata mimi nimecheza
naye ili kuimarisha kikosi changu na kumtumia kama kocha wa uwanjani,” alisema
Maxime.
Naye Kocha Msaidizi wa Mtibwa, Zuberi Katwila
alisema: “Mgosi tumemsajili kwa kuwa tunajua atatusaidia msimu ujao, tumempa
mkataba wa mwaka mmoja.”








0 COMMENTS:
Post a Comment