Na Wilbert Molandi
KUONDOKA kwa kiungo mshambuliaji wa Simba,
Mwinyi Kazimoto (pichani kushoto) kumeikosesha Klabu ya Simba mamilioni kutokana na kuelezwa
kuwa, mchezaji huyo alikuwa akitakiwa na Klabu ya FC Porto ya Ureno.
Kazimoto amesaini mkataba wa kuichezea
Al-Markhiya Sports Club ya Qatar, wiki hii kwa dau la dola 50,000 (Sh milioni
80), ikiwa ni mkataba wa mwaka mmoja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,
Zakaria Hans Pope amesema kiungo huyo amechukua maamuzi ya haraka lakini kama
angeendelea kubaki Simba kwa muda, angepata dili hilo la kusajiliwa na klabu
hiyo ya Ureno ambao anadai walitoa ahadi ya kutoa donge nono zaidi.
“Kazimoto amechukua maamuzi ya haraka ya
kwenda kucheza soka la kulipwa Qatar, alitakiwa kusubiri kutokana na ofa
tulizokuwa tunazipata kutoka Ulaya.
“FC Porto ilionyesha nia ya kumsajili hivi
karibuni, lakini akatoroka na kwenda huko Qatar kwenye majaribio, timu hiyo
iliahidi kutoa dau kubwa la usajili na mshahara zaidi ya huo atakaoenda kuupata
Qatar,” alisema Hans Pope.








0 COMMENTS:
Post a Comment