Mo Farah wa Uingereza ameonyesha sasa ni moto wa kuotea mbali
baada ya kushinda mbio za mita 10,000 katika ubingwa wa dunia jijini Moscow,
Urusi.
Farah ameshinda mbio hizo na kumuacha Jeilan wa Ethiopia ambaye
miaka miwili iliyopita alimshinda Farah.
Pamoja na kushinda mbele ya Jeilan, Farah ambaye ni Mwingereza
mwenye asili ya Somalia ameweka rekodi kwa kuwa hakuna mwanariadha wa Uingereza
aliwahi kushinda mbio hizo kwa urefu huo.














0 COMMENTS:
Post a Comment