TANGAZO LA LIGI KUU ENGLAND NCHINI MAREKANI... |
Kiungo nyota wa Tottenham Hotspurs, Gareth
Bale amekata mzizi wa fitna baada ya kumtamkia kocha wake Andre Villas-Boas
kwamba anataka kuondoka.
Awali ilikuwa inaonekana kama hadithi
na AVB ndiye alibaki tegemeo pekee la Bale kubaki Spurs kwa kuwa ni rafiki
yake, lakini yeye sasa amemaliza kazi.
Bale amemuambia AVB katika siku yake ya
kwanza mazoezini kwamba anataka kuondoka zake na kwenda Real Madrid.
Maneno hayo yamekuwa kama kidonda kwa
AVB ambaye ndiye alikuwa tumaini la Spurs kumbakiza Bale ambaye Real Madrid
imefikia hadi dau la pauni milioni 85 ambalo ni kubwa zaidi kuwahi kutokea
duniani katika uhamisho.
Kwa kauli hiyo ya Bale kwa AVB, hali
halisi ‘inajichora’ kwamba hakuna ujanja, msimu huu lazima atajiunga na vigogo
hao wa Hispania.
BALE AKIONDOKA MAZOEZINI... |
0 COMMENTS:
Post a Comment