August 22, 2013





Mshambuliaji mpya wa Barcelona, Neymar ameikoa timu hiyo kulala katika mechi ya Kombe la Super Cup baada ya kuifungia bao la kusawazisha.


Mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, David Villa alikuwa wa kwanza kuifungia Atletico Madrid na Neymar aliyeingia akitokea benchi akasawazisha hivyo kufanya matokeo kuwa 1-1.



Wakati Barcelona inapata sare hiyo, mshambuliaji wake Lionel Messi alitolewa baada ya kupata matatizo ya misuri na imeelezwa atafanyiwa uchunguzi zaidi.

Mechi ya pili itapigwa Jumatano ijayo kwenye dimba la Vicente Calderon safari hii Atletico Madrid wakiwa nyumbani.




Bao hilo la Neymar limekuwa la kwanza la mashindano akiwa na Barcelona aliyojiunga nayo akitokea Santos ya kwao Brazil.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic