August 25, 2013

  
NURDIN (KATIKA) AKIWA NA WACHEZAJI WENGINE WA RHINO DAKIKA CHACHE KABLA YA MECHI YA SIMBA JANA
Kiungo mpya wa Rhino Tabora, Nurdin Bakari, jana alikuwa mmoja wa wachezaji waliong’ara katika mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Nurdin alikuwa msumbufu kwa viungo na mabeki wa Simba.


Wakati fulani mashabiki kwenye uwanja huo walikuwa wakimshangilia Nurdin kutokana na uwezo aliokuwa akionyesha.

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2 huku Nurdin akiwa kati ya wachezaji waliofanya vizuri sana.

Baada ya mechi, wachezaji wengi wa Simba walimfuata na kumpongeza kutokana na mchezo mzuri aliouonyesha.


Kabla ya kutua Rhino, Nurdin alikuwa mmoja wa wachezaji tegemeo wa Yanga ambayo alijiunga nayo akitokea Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic