Kocha
msaidizi wa zamani wa Man City, David Platt amesema walikuwa na mpango wa kumtema
kipa wao namba moja Joe Hart.
Platt
mmoja wa mabeki nyota zamani wa Arsenal, amesema mpango huo ulikuwa hivi;
kumtema Hart na kumsajili, Asmir Begovic anayekipiga Stoke City.
Akizungumza
na runinga ya Al Jazeera, Platt alisema uamuzi huo ulitokana na makosa lukuki
aliyokuwa akifanya Hart.
“Kama
mimi na Mancini tungekuwa Man City hadi sasa, basi sasa hivi Hart asingekuwepo.
Tuliona amekuwa na makosa mengi sana, hivyo tulipanga kumsajili Begovic
kuchukua nafasi yake,” alisema.
Kauli
hiyo ya Platt imeonyesha kuwashtua wengi lakini imeubua mjadala wa makosa mengi
ya kila huyo katika mechi kadhaa zikiwemo zile za England pamoja na ile ya juzi
dhidi ya Cardiff ambayo Man City ililala kwa mabao 3-2.
0 COMMENTS:
Post a Comment