Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete ni
kati ya wachezaji watatu walioanza kwa kasi kuwania kiatu cha dhahabu katika
msimamo wa wafungaji wa Ligi Kuu Bara.
Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama baada
ya kila timu kucheza mechi mbili na Tegete, kiungo Jonas Mkude wa Simba na
mshambuliaji Bakari Kondo, kila mmoja ana mabao mawili.
Wachezaji hao watatu ndiyo wanaoonyesha
kuianza kwa kasi kazi ya ufunagaji mabao katika ligi hiyo ambayo itasimama hadi
Taifa Stars itakapocheza na Gambia.
Ligi hiyo inayosimama kwa wiki mbili,
itaanza kutimua vumbi tena Septemba 14 na huenda kasi ya yupi ataendelea zaidi
itaonekana tena.
Lakini sasa watatu hao, wanaendelea
kubaki kileleni baada ya mechi hizo mbili za mwanzo wa ligi hiyo inasubiriwa
kwa hamu.
Kwa upande wa msimamo wa timu, JKT Ruvu
imekaa kileleni kwa kuwa na pointi sita na inafuatiwa na Yanga, Azam FC, Coastal
Union, Simba na Mtibwa Sugar ambazo kila moja zina pointi nne lakini
zinapishana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment