Mtangazaji maarufu wa michezo nchini
Abdallah Majura amesema yuko salama na anaendelea vizuri na kazi zake.
Majura amesema hayo punde katika
mahojiano yaliyofanyika dakika kumi zilizopita akieleza namna alivyopata
usumbufu baada ya kuzushiwa kifo.
“Niko Dodoma naendelea na shughuli
zangu, hakika nimepata usumbufu mkubwa sana,” alisema Majura mmiliki wa kituo
cha redio cha ABM FM.
“Nimesikia kuna mhadhiri wa chuo cha
Diplomasia ndiye amefariki, majina yetu yanafanana na mara nyingi sana watu
walikuwa wakitufananisha kupitia majina.
“Sasa watu wakajua ni mimi na
wamenipigia simu nyingi sana hadi nilitamani nizime. Lakini mashukuru Mungu
niko vizuri na naendelea na kazi zangu.”
Majura aliwataka ndugu jamaa na rafiki
zake kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
“Unajua hadi watu jukwaa la wahariri
walishaanza kujipanga namna ya kuendesha msiba wangu. Lakini waliponipigia
wakanipata na tukazungumza.
“Sasa sijui kwa nini imehamia kwangu kwa
watu kuamini hivyo lakini kifupi naweza kusema namshukuru Mungu niko salama tu.”
0 COMMENTS:
Post a Comment