NYAMLANI (MWENYE TAI) |
Wagombea wawili, Athumani Nyamlani na Jamal Malinzi
wamepitishwa kuwania nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
MALINZI |
Malinzi na Nyamlani ambaye anashikilia nafasi ya Makamu
wa Kwanza wa Rais wa TFF, wamepitishwa baada ya usaili uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Upinzani kati ya Nyamlani na Malinzi umekuwa mkali sana
tokea walipotangaza tu kugombea.
Katika nafasi hiyo kulikuwa na wagombea wanne na wawili
kati yao hawakupita ambao ni Omary Mussa na Richard Lukambula.
Kwa upande wa umakamu wa urais, Wallace Karia, Nassib Ramadhani na Iman
Madega, mwenyekiti wa zamani wa Yanga, ndiyo waliopitishwa kuwania nafasi hiyo.
Wakati huohuo, usaili huo pia umemng’oa Shaffi Dauda
aliyekuwa nawania ujumbe.
0 COMMENTS:
Post a Comment