AC Milan
imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Cagliari katika mechi ya Sera A
kwenye Uwanja wa San Siro jijini Milan, Italia.
Milan imeibuka
na ushindi huo huku mshambuliaji wake Mario Balotelli akifunga bao la tatu kwa
shuti kali baada ya krosi nzuri iliyopigwa na Abate kutua kichwani mwa beki wa
Cagliari kabla ya kumfikia yeye.
Kabla ya hapo,
Milan ilipata mabao yake mawili kupitia kwa Robinho katika dakika ya 8 na
Mexes, dakika ya 31 kabla ya Balotelli kumaliza kazi dakika ya 62. Kabla wageni
hao walipata bao lao kupitia Marco Sau.
Pamoja na
ushindi huo, Balotelli alicheza vizuri mechi hiyo iliyomalizika punde na kuwa
msumbufu kwa mabeki wa Cagliari.
0 COMMENTS:
Post a Comment