POULSEN |
Kocha
Poulsen amesema Gambia ilistahili kushinda kwa vile ilitengeneza nafasi nyingi
kuliko timu yake, na kuongeza kuwa mabao iliyopata Gambia yalikuwa mepesi.
“Hatukutengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini tukaruhusu mabao
mapesi. Nawapongeza Gambia kwani walistahili ushindi. Unapofanya makosa
unaadhibiwa. Gambia ilikuwa timu nzuri leo, kwani ilitengeneza nafasi nyingi za
kufunga, sisi tukatoa mabao mepesi,” amesema Kim.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imemaliza
katika nafasi ya tatu katika kundi hilo lililokuwa na timu nne ikiwa na pointi
sita ilizozipata nyumbani kwa kuzifunga Morocco na Gambia.
Hata hivyo, Kim amesema sababu nyingine ya kutofanya vizuri ni
kuwakosa wachezaji wanaocheza nje ya nchi na wengine wa kikosi cha kwanza ambao
ni majeruhi.
Mabao yote ya Gambia katika mechi hiyo iliyochezeshwa na Munyemana
Hudu kutoka Rwanda yalifungwa na nahodha wa timu hiyo Mustapha Jarjue. Alifunga
la kwanza dakika ya 44 na kupachika lingine dakika ya 51, mabao yaliyotokana na
wachezaji wa Stars kutokuwa makini.
Katika mechi hiyo Stars iliwakilishwa na Juma Kaseja, Vincent
Barnabas, Erasto Nyoni/David Luhende, Nadir Haroub, Henry Joseph, Frank Domayo,
Haruni Chanongo, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Simon Msuva na Khamis Mcha/Juma
Liuzio.
Taifa Stars inaondoka Banjul kesho (Septemba 8 mwaka huu) saa 6
mchana kwa ndege ya Arik hadi Dakar, Senegal ambapo itaunganisha kwa ndege ya
Kenya Airways kupitia Nairobi ambapo itawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) kesho, saa 8.05 mchana.
0 COMMENTS:
Post a Comment