Simba imefanikiwa kuwafunga Mafunzo ya Zanzibar kwa
mabao 4-3 katika mkali wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam.
Simba imewafunga Mafunzo katika mechi hiyo maalum ya
kuwatambulisha wachezaji wake watatu, Gilbert Kaze ‘Demunga’ na Amis Tambwe
ambao ni raia wa Burundi.
Mwingine aliyekuwa anatambulishwa katika mchezo huo wa
leo alikuwa ni Henry Joseph, kiungo kutoka Kongsvinger ya Norway ambaye
amerejea Msimbazi.
Mechi ilikuwa kali ya kuvutia na jumla ya mabao saba
yamefungwa katika dakika 90 na kufanya mambo yawe ya kuvutia.
Mabao ya Simba yalifungwa na Tambwe mwenye ambaye
alipachika mawili, halafu Sino Augustino na Said Nassor ‘Chollo’ akafunga la
nne.
0 COMMENTS:
Post a Comment