October 31, 2013


Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe ameonyesha kuchanganyikiwa na kushindwa kuzungumza.


Tambwe raia wa Burundi alilazimika kutimua mbio pamoja na wachezaji wengine wa Simba pia wale wa Kagera Sugar, sekunde tu baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya mwisho ya mchezo wa leo kati yao.

Mashabiki wa Simba walianza kufanya vurugu wakipinga penalty iliyotolewa na mwamuzi huyo na Kagera wakasawazisha bao.
Wakati wachezaji wanakimbilia vyumbani, Tambwe alikataa kuzungumza huku akionekana ni mwenye hofu.

Katika mechi hiyo, Tambwe alizidi kujichimbia kileleni kwa kufunga bao la tisa.

Tambwe amefunga bao la tisa, siku moja tu baada ya Hamisi Kiiza wa Yanga, raia wa Uganda kufikisha mabao nane.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic