Kocha wa zamani wa Simba, Milovan
Cirkovic amesema wakati akiwa katika mazungumzo na timu kadhaa amekuwa
akiendelea na kilimo.
Milovan kwa kushirikiana na mkewe
aliyezaa naye watoto watatu, amekuwa akifanya kazi mbalimbali za kilimo cha
apple.
“Kawaida kabisa kufanya kazi kama hizi,
ndiyo maisha ya hapa Cacak,” alisema Milovan aliyewahi kuinoa Simba.
Milovan ndiye kocha aliyeiongoza Simba
kutoa kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya Yanga, rekodi ambayo ni kubwa zaidi kwa
kipindi cha zaidi ya miaka 15 kwa watani hao.
0 COMMENTS:
Post a Comment