Kiingilio cha chini kwenye mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi
(Oktoba 20 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000. Kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi
ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kwa upande wa viti vya rangi ya
bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP
C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748
tu tiketi moja itapatikana kwa sh. 30,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo
utakaoanza saa 10 kamili jioni katika vituo mbalimbali.
Vituo hivyo ni Shule ya Sekondari
Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora,
Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na
BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Mechi hiyo namba 63 itachezeshwa
na Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam, ambapo atasaidiwa na Hamis Changwalu wa
Dar es Salaam pia, na Ferdinand Chacha wa Bukoba. Mwamuzi wa akiba ni Oden
Mbaga wa Dar es Salaam.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa John Kiteve kutoka
Iringa wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Stanley Lugenge wa
Njombe.
0 COMMENTS:
Post a Comment