October 8, 2013




Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amemcharukia mshambuliaji wake, Jerry Tegete na kumtaka abadilike.

Brandts raia wa Uholanzi amemtaka Tegete kubadilika na kujenga tabia ya kujituma.


Katika mazoezi ya leo kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Mabibo jijini Dar, Tegete alionyesha mabadiliko na kucheza kwa kujituma zaidi.

“Kweli nilikasirika sana, Tegete amekuwa hajitumi kama ilivyokuwa mwanzo. Lakini sasa mambo yamebadilika kidogo.

“Kweli ana uwezo, lakini ameshindwa kabisa kujituma kitu ambacho si sahihi. Utaona niliamua kumuweka benchi katika mechi zilizopita kutokana na suala hilo. Ila sasa anaonekana kuelewa nilichomueleza,” alisema.

Katika mechi mbili zilizopita ambazo Yanga ilishinda 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting na 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, Tegete alikaa benchi na Hamis Kiiza akaanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic