October 9, 2013





Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts ametibuana na beki wake, Kelvin Yondani na kumuondoa kuendelea na mazoezi.


Katika mazoezi ya timu hiyo leo kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Royola jijini Dar, Brandts amemtaka Yondani kuondoka ndani ya uwanja baada ya kutofanya alichokuwa anamuelekeza.

Brandts alitaka Yondani akimbie kwa kasi zaidi, lakini yeye hakufanya hivyo, akachukua uamuzi wa kumuondoa mazoezini.
“Kweli nimefanya hivyo kwa kuwa namsisitiza kukimbia kwa kasi ya juu na yeye anakimbia taratibu, nimerudia lakini bado hakufuata. Nimeona vema akatupisha,” alisema Brandts.

Baada ya kutoka uwanjani, Yondani aliamua kuondoka zake katika eneo hilo, na baada ya mazoezi, Brandts alimuulizia na kuelezwa ‘aliishasepa’.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic