Kiungo nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima
ameunguliwa na nyumba yake.
Nyumba anayoishi iko Magomeni jijini Dar
es Salaam na moto huo ulianza saa 12 alfajiri hadi ulipozimwa na majirani saa
moja asubuhi leo.
Taarifa zinasema nyumba hiyo imeungua
kutokana na hitilafu ya umeme katika moja ya nyanya ndani ya nyumba hiyo.
Vitu kadhaa vya thamani ndani ya nyumba
yake vimeteketea kwa moto lakini familia yake imesalimika baada ya majirani
kuwaokoa.
“Kweli ninawashukuru sana majirani kwa
kuonyesha uungwana wa hali ya juu, bila ya wao nyumba yote ingeungua.
“Lakini kuna vitu vichache vimefanikiwa
kutoka ila vingi sana vimeungua na moto huo uliokuwa mkali sana,” alisema.
Hadi blogu hii inaondoka eneo la tukio
asubuhi hii, baadhi ya watu na mashabiki wa Yanga walikuwa wamefika kwa ajili
ya kutoa msaada zaidi.
Pia fundi wa umeme alikuwa anasubiriwa
ili kuangalia hitilafu iliyosababisha moto ilitokana na kitu gani.
0 COMMENTS:
Post a Comment