Baada ya kupatikana
na kesi ya kujibu kwenye mashitaka manne ya wizi wa shaba yenye thamani ya
zaidi ya milioni 360, inayomkabili aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Simba,
Hassan Othman ‘Hassanoo’ leo iliendelelea kwenye Mahakama ya Kisutu jijini Dar
es Salaam.
Hassanoo aliyekuwa
kiongozi na mmoja wa wadau maarufu wa Wekundu wa Msimbazi alijitetea na kuomba mahakama
hiyo imfututie mashitaka.
Alidai katika mashahidi
15 waliofika kwenye kesi hiyo kutoa ushahidi hakuna yeyote aliyemhusisha moja
kwa moja kuhusika na wizi huo.
Kesi hiyo imeahirishwa
na Hassanoo amerudishwa rumande, sasa itatajwa tena mahakamani hapo Oktoba 11,
mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment