Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayoongozwa na Jaji wa Mahakama ya
Rufani Tanzania, Bernard Luanda itakutana keshokutwa (Oktoba 10 mwaka huu)
kusikiliza rufani zilizowasilishwa mbele yake.
Waombaji uongozi watatu wamekata
rufani katika Kamati ya Jaji Luanda wakipinga kutopitishwa kugombea katika
uchaguzi wa TFF, uamuzi uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa ajili ya
uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Warufani ni Samwel Nyalla
aliyeondolewa kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda namba 2 ya
mikoa ya Mara na Mwanza kwa kutojaza kikamilifu fomu namba 1 ya maombi ya
kugombea uongozi TFF kwa kutoonesha malengo yake.
Ayoub Nyaulingo yeye anapinga
kuondolewa kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda namba 6 (Katavi
na Rukwa) kwa kutokuwa na uzoefu uliothibitika wa miaka mitano katika uongozi
wa mpira wa miguu.
Naye Ayoub Nyenzi amekata rufani
kupinga kuondolewa kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha Kanda
namba 7 (Iringa na Mbeya) kwa kushindwa kuthibitisha uraia wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment