October 7, 2013




Kiungo wa AS Cannes ya Ufaransa, Shomari Kapombe, amebakiza siku saba kabla ya kurejea uwanjani na kuanza mazoezi.


Mmoja wa watu walio katika Kitengo cha Afya cha AS Cannes ambaye hujitambulisha kwa jina moja la Pierre, amesema kuwa Kapombe ataanza mazoezi ndani ya siku saba.

“Anaendelea vizuri sana na mategemeo ni kuanza mazoezi ndani ya siku saba, hata hivyo atakuwa akifanya taratibu kwanza kabla ya kuungana na wenzake.

“Hatutamruhusu afanye mazoezi magumu, lakini anaweza kucheza na wenzake kama watakuwa katika kipindi cha mazoezi ya kawaida,” alisema.

Kapombe alifanyiwa upasuaji wa kidole cha mguu ikiwa ni takribani wiki tatu tu baada ya kujiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ufaransa.

Kwa sasa timu hiyo inashika nafasi ya tatu katika ligi hiyo ikiwa na pointi 16 nyuma ya Monaco 2 na vinara Marseille Consolat, kila moja ikiwa na pointi 19.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic