Mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza amemwambia Kocha wa Mkuu wa timu hiyo,
Ernest Brandts kuwa kama anataka mabao basi ampange namba 10 na siyo 11.
Awali,
kocha huyo raia wa Uholanzi alitangaza kumtumia Ngassa pembeni akicheza namba
11, lakini katika mechi za hivi karibuni anamchezesha 10.
Akizungumza
na Championi Jumatatu, Kiiza alisema katika mechi na Mtibwa Sugar ameshindwa
kufunga bao kutokana na kuchezeshwa namba 11.
Kiiza alisema,
ana uwezo wa kucheza nafasi hizo zote, lakini katika msimu anataka kucheza
namba 10 ili afunge mabao mengi ili atimize malengo yake ya kuchukua ufungaji
bora kwenye msimu huu.
“Nina
uwezo wa kucheza namba 7, 10 na 11, lakini kwenye msimu huu ninataka kocha
anitumie kucheza namba ili nifunge mabao mengi kwenye msimu huu.
“Malengo
yangu ni kuchukua ufungaji bora wa msimu huu, kwenye mechi mbili hizi
tulizocheza dhidi ya Mtibwa Sugar na Kagera Sugar nimechezeshwa namba 11,
lakini ninaomba nichezeshwe 10 ili nifunge mabao,” alisema Kiiza.
0 COMMENTS:
Post a Comment