October 14, 2013





Jezi namba 17 ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa zimeongoza kwa mauzo Kagera kutokana na mashabiki wengi kuzigombania kwa ajili ya kuzinunua.

Ngassa ambaye msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara alirejea kwenye timu hiyo akitokea Simba baada ya kumaliza mkataba wa kukipiga katika klabu hiyo.


Salehjembe lilishuhudia jezi za kiungo huyo zikinunuliwa kwa wingi nje na ndani ya Uwanja wa Kaitaba wa Kagera wakati timu ilipovaana na Kagera Sugar.

Jezi hizo zilikuwa zinauzwa shilingi Elfu Kumi zilizotandazwa chini na nyingine kutundika kwenye miti.

Wauzaji wa jezi hao walisikika kuzipigia kwa wingi tyofauti na jezi nyingine ya Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.
Mmoja wa wauzaji wa jezi hizo, Mohamed Issa alisema “Jezi zilizopo kwenye soko hivi sasa ni Ngassa ambazo tunaziuza sana tofauti na za wachezaji wote wa Yanga.
“Hata kwenye mechi ya leo, unaona mashabiki wanavyozinunua, kiukweli wanazipenda na hiyo imetokana na kurejee kwenye timu yake ya zamani,” alisema Issa.
mwisho

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic