Kocha wa Barcelona, Tata Martino amesema kama watafungwa katika mechi dhidi ya ya Celtic leo usiku, hawatakuwa na kisingizio cha kukosekana kwa Lionel Messi.
Tata amesema wana kikosi kizuri na imara na wana uwezo wa kufanya vizuri katika mechi hiyo pamoja na kwamba wanamkosa Messi ambaye ni majeruhi.
"Huu si wakati wa kutanguliza visingizio kama itatokea tumepoteza mchezo dhidi ya Celtic. Messi ni mtu muhimu sana kwetu.
“Lakini tuna kikosi ambacho kina uwezo wa kushinda mechi nyingi na kwa uhakika, hivyo tunachotakiwa ni kushinda bila ya kujali ugumu wa mechi yenyewe,” alisema Tata raia wa Argentina.
Messi aliumia katika moja ya mechi za La Liga na analazimika kuikosa mechi hiyo ikiwa ni mara ya pili kukosa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu kutokana na kuwa majeruhi.
0 COMMENTS:
Post a Comment