October 1, 2013




Bingwa wa dunia  wa IBF, Francis Cheka amesema anajivunia kutokana na uamuzi wake wa kwenda shule.

Cheka ameamua kurejea shuleni na kusoka kidato cha kwanza hadi cha nne.
 
Akizungumza na blogu hii, Cheka alisema amekuwa akitamani siku zote kuingia darasani.

“Sikuwahi kuficha, nilikuwa nikisema siku zote kwamba sikusoma na nilitamani kwenda darasani.

“Sasa nimefanikiwa, kweli  ninashukuru sana na nitakuwa ninajityuma sana licha ya kwamba kuna ugumu kutokana na majukumu ya kifamilia na kazi zangu,” alisema Cheka.

Cheka amekuwa mwanamichezo wa pili kukubali kurejea darasani licha ya kuwa na umri mkubwa. Wa kwanza alikuwa mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali ‘Field Marshal’.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic