MWISHO WA DAKIKA 90
Dk 90, inaonekana hata Mgambo
wamekata tamaa
Dk 85&89, Yanga wanatumia
muda mwingi kugongeana wakionyesha kuridhika na tatu bila.
Dk 84 Mgambo wanafanya
shambulizi lakini mpira unaishia mikononi kwa kipa wa Yanga, Dida.
Dk 79 Nusura Tegete afunge
lakini kipa wa Mgambo anawahi mpira
Dk 72 Ngassa anatolewa na Tegete anaingia
kuchukua nafasi yake ni baada ya kuumia.
Dk 69, Ngassa anapiga shuti
kali lakini kipa wa Mgambo anaokoa na kuwa kona.
GOOOOO Dk 67 Kavumbagu amafunga
bao la tatu baada ya kuiwahi krosi ya Simon Msuva aliyepiga mbele ya mabeki
wawili wa Mgambo.
Dk 61, Kavumbagu anapoteza
nafasi ya kfuunga akiwa yeye na kipa
GOOOO Dk 50 Hamis Kiiza
anapiga mkwaju huo na kuandika bao la pili.
PENAAAAAT.. Dk 48 Kavumbagu
anaangushwa ndani ya eneo la hatari na kipa wa Mgambo
Dk 46 Yanga wanaanza kwa kasi sana kipindi cha
pili na Ngassa anaonekana ni tatizo kwa mabeki wa Mgambo
Dk 5. Mchezo umeanza kwa kasi
na Mgambo Shooting wanaonekana wamepania kushinda.
Dk 11 Yanga wanaanza
kubadilika na kupeleka mashambulizi mfululizo na Mgambo wanaonekana kuzidiwa.
GOOOOO Dk 31 Mbuyu Twite
anaifungia Yanga bao la kwanza kwa shuti kali kutokana na mpira wa adhabu.
Dk 38 Kavumbagu anashindwa
kufunga baada ya pasi nzuri ya Ngassa.
Dk 42, Ngassa nusura aifungie
Yanga bao lakini shuti lake linaokolewa.
HALF TIME
0 COMMENTS:
Post a Comment