Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji alitumia zaidi ya dakika 10 akiteta pembeni na manahodha
wawili wa kikosi cha Yanga.
Manji
ambaye alifika kwa kushtukiza wakati Yanga ikifanya mazoezi katika Gym ya Rio
katika jumla la biashara la Quality Centre alitumia muda huo kuzungumza na
Athumani Idd ‘Chuji’ na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Muda
mwingi mwenyekiti huyo alionekana kufafanua jambo wakati akizungumza na manahodha
hao.
Baada
ya mkutano huo wa kushtukiza, Cannavaro na Chuji walijibu kifupi kwamba
walikuwa wanazungumzia masuala ya klabu tu.
“Mambo
ya kikosi na klabu kwa ujumla,” alisema Cannavaro.
Naye
Manji alisema: “Mambo yetu ya ndani ya Yanga, sidhani ni vizuri kuyaweka kwenye
vyombo vya habari. Mimi ni mwenyekiti na pale nilikuwa nazungumza na manahodha.”
0 COMMENTS:
Post a Comment